
Klabu ya Paris Saint-Germain imetangaza kuwa supastaa wa Brazil, Neymar atakuwa nje ya uwanja kwa muda uliosalia wa msimu huu baada ya kufanyiwa upasuaji wa kifundo cha mguu.
Neymar atakosa mchezo muhimu wa 16 bora ya ligi ya mabingwa barani Ulaya UEFA kesho jumatano dhidi ya Bayern Munich. Na sasa ni rasmi kuwa Neymar atakuwa nje ya uwanja kwa muda wa miezi mitatu hadi minne ijayo.