
Ligi kuu soka Tanzania bara NBC Premier league itakuwa kibaruani leo kwa mchezo mmoja mnyama Simba SC watawaalika matajiri wa Chamazi Azam FC katika dimba la Benjamin Mkapa Dar es Salaam saa 1 kamili.
Kaimu msemaji wa Azam, Hashim Ibwe amekiri ugumu wa mchezo wa leo dhidi ya wapinzani simba hasa mara baada ya kutoka katika michuano ya kimataifa na kutokuwa na kuendelezo wa matokeo mazuri lakini licha ya ugumu huo wako tayari kuchukua alama tatu mbele ya mnyama hii leo pale Benjamini Mkapa.
Kwa upande wake kocha wa Azam, Kally Ongala yeye amesema wachezaji wapo tayari kwa asiilimia 100 kuwakabili Simba katika mchezo huo.
Kuelekea mchezo huo msemaji wa klabu ya Simba, Ahmed Alli amesema hakuna wanachohitaji zaidi ya alama tatu katika mchezo wa leo na kubainisha kuwa kikosi cha Simba kipo kamili isipokuwa wataendelea kukosa huduma ya winga Augustine Okrah.