
Mwenyekiti wa Bodi ya Wadhamizi ya Chadema, Sylvester Masinde amefariki dunia katika Hospitali ya Rufaa ya Bugando jijini Mwanza alipokuwa anapatiwa matibabu.
Taarifa ya tanzia iliyotolewa na Chadema na kusainiwa na Katibu Mkuu wa chama hicho, John Mnyika imeeleza Masinde amefariki dunia leo marchi 15.