fbpx

Mwanaume ahukumiwa miaka 30 baada ya kukubali kulawitiwa

Mwanaume afungwa jela baada ya kukubali kulawitiwa

Mahakama ya Wilaya ya Newala Mkoani Mtwara imemhukumu kifungo cha miaka 30 Jela, Selemani Mustafa Mtipa maarufu kama Sele Mkazi wa Wilaya hiyo baada ya kumtia hatiani na kukiri kutenda kosa la kuruhusu kuingiliwa kinyume na maumbile na Wanaume mbalimbali.

Hukumu hiyo imetolewa na Hakimu Mkazi Mwandamizi/Mfawidhi Innocent Sotter mbele ya Mwendesha Mashtaka wa Serikali, Salehe Mganga baada ya Mshtakiwa kukiri kutenda kosa hilo, kwa nyakati tofauti.

Mshitakiwa huyo ameadhibiwa kwa kosa la kuruhusu kuingiliwa kinyume na maumbile kinyume na kifungu nambari 154 kifungu kidogo cha kwanza (1)(c) cha kanuni ya adhabu sura na 16 iliyofanyiwa marejeo ya mwaka 2022.

  • https://cast3.asurahosting.com/proxy/jambocom/stream

Verified by MonsterInsights