
Mwanamke mmoja aliefahamika kwa jina la Monica Patrick (31) mkazi wa wilaya ya Itilima mkoa wa Simiyu amekutwa amefariki dunia kwa kuuwawa.
Kisha mwili wake kudumbukizwa kandokando ya kichaka kilichopo pembezoni mwa ziwa Victoria katika mtaa wa Kinyang’wena Manispaa ya Musoma mkoani Mara huku chanzo cha kifo chake kitajwa kupewa dawa na mganga wa kienyeji kwa lengo la kumsaidia katika shughuli zAke za madini.
Wakizungumza na Jambo FM baadhi ya wananchi waliokuwa katika eneo hilo ambapo mwanamke huyo ametupwa nadani ya maji baahi ya wananchi hao wakazungumza. Mbali na tukio hilo la mwanamke huyo kukutwa katika kichaka hicho akiwa amefariki mmoja wa wakazi hao akatoa ombi kwa serikali kukamilisha ujenzi wa mradi wa maji taka katika eneo hilo kwani kwa sasa limegeuka kuwa eneo la kutupia maiti.
Akithibitisha kutokea kwa tukio hilo kamanda wa jeshi la zima moto na uokozi mkoa wa Mara, Mrakibu Agustine Magere amesema kuwa walipokea simu ya kwenda kufanya uokozi.