fbpx

Mwanafunzi wa darasa la nne adaiwa kujinyonga

Mwanafunzi wa darasa la nne shule ya msingi Kambarage halmashauri ya mji wa Kibaha, mkoa wa Pwani, Tatu Machemba amepoteza maisha ikielezwa kuwa amejinyonga kwa kutumia kamba chumbani nyumbani kwao mtaa wa mkoani mjini Kibaha, Pwani.

Mwenyekiti wa mtaa wa mkoani, Shabani Rashidi amesema kuwa taarifa za tukio hilo zilimfikia jumapili kwa njia ya simu na kabla ya kwenda aliwasiliana na jeshi la polisi.

Amesema baada ya kufika eneo la tukio waliingia na kukuta mwili wa mwanafunzi huyo kichwa chake kimechomekwa kwenye kamba na yeye amepiga magoti. Mwenyekiti huyo amesema kinacholeta maswali kwa baadhi ya wananchi ni mazingira yaliyokutwa kwani mwili wa marehemu haukuwa unaning’inia bali alikutwa amepiga magoti. Akizungumza kwa njia ya simu kamanda wa polisi mkoani Pwani, Piusi Lutumo amekiri kuwepo kwa tukio hilo na kueleza kuwa litafanyia uchunguzi zaidi.

Mwili wa marehemu umehifadhiwa hospitali ya rufaa mkoa wa Pwani Tumbi kwa ajili ya utaratibu kabla ya kukabidhiwa kwa ndugu.

  • https://cast3.asurahosting.com/proxy/jambocom/stream

Verified by MonsterInsights