
Mwanafunzi wa kidato cha kwanza katika shule ya sekondari Mwinuko iliyopo kata ya Kitangiri wilaya ya Ilemela jijini Mwanza, Grolia Faustine amefariki kwa kudondokewa na jiwe wakati akichimba mchanga kama adhabu aliyopewa shuleni hapo huku mwenzie aliyekuwa naye akivunjika mguu.
Akieleza kuhusu tukio hilo shuhuda, Frank Isaya ambaye pia ni mwanafunzi wa kidato cha kwanza amesema walipewa adhabu hiyo na mwalimu mkuu kwa kosa la kuzungumza lugha ya kiswahili tofauti na taratibu za shule hiyo zinazowataka kuongea lugha ya kiingereza kwenye maeneo ya shule ambapo yeye baada ya kuona jiwe linataka kudondoka alifanikiwa kukimbia na likamdhuru mwenzie kwa kumdondokea kichwani.