
Jeshi la Polisi mkoa wa Geita linamshikilia Samweli Subi , ambae Ni mwalimu wa shule ya msingi Igaka kwa tuhuma za kumuua mwalimu mwenzie Emmanuel Chacha maarufu kwa jina la Dizzo kwa kumchoma kisu akiwa anasimamia mitihani ya KKK ya darasa la kwanza.
Kamanda wa Jeshi la Polisi mkoa wa Geita, Safia Jongo amethibitisha kutokea kwa tukio hilo na mtuhumiwa tayari amekamatwa na kukiri kutekeleza tukio hilo huku chanzo kikihusishwa kugombea nafasi ya uongozi.