
Lance Reddick, muigizaji wa filamu ambaye alibobea katika kuigiza kama magwiji wakubwa, wakali na pengine wabaya kwenye TV na filamu, ikiwa ni pamoja na “The Wire,” ″Fringe” na filamu za “John Wick”, amefariki dunia. Alikuwa na miaka 60.
Reddick alikufa “ghafla” Ijumaa asubuhi, mtangazaji wake Mia Hansen alisema katika taarifa, akihusisha kifo chake na sababu za asili. Hakuna maelezo zaidi yaliyotolewa.
Mongozaji wa filamu ya “John Wick – Chapter 4” Chad Stahelski na nyota Keanu Reeves walisema waliweka wakfu filamu ijayo kwa Reddick na “wamehuzunishwa sana na kuvunjika moyo kwa kumpoteza.”