
Msumbiji imerekodi ongezeko la idadi ya wagonjwa wa kipindupindu katika wiki chache zilizopita, Shirika la Afya Ulimwenguni limesema katik taarifa yake yah apo jana Jumatano, licha ya nchi zingine nyingi za Kiafrika zikiripoti kupungua maambukizi.
Msumbiji imepokea idhini ya kuongeza dozi milioni 1.3 za chanjo ya kipindupindu kusaidia kudhibiti kuenea kwa maradhi hayo, shirika hilo lilisema, wakati wakifanya juhudi za kukabili uhaba wa chanjo.
Jirani yake Msumbiji Malawi, ambayo ambayo kwa sasa inakabiliwa na kimbunga kilichosababisha mamia wakipoteza Maisha nayo inapambana na mlipuko mbaya zaidi wa kipindupindu katika historia yake, lakini sasa walau inashuhudia kupungua kwa visa na vifo, afisa wa shirika la afya ulimwenguni WHO na mtaalamu wa magonjwa ya mlipuko Dk Otim Ramadan amesema.