fbpx

Msichana achomwa kisu hadi kufa na watu wasiojulikana

Binti mwenye miaka 12 mkazi wa mtaa wa Pasiansi juu manispaa ya Ilemela jijini Mwanza amefariki kwa kuchomwa kisu na watu wasiojulikana ambao inadaiwa walimvamia usiku wa manane nyumbani anapoishi na bibi yake wakambaka kisha wakamchoma kisu shingoni na kupelekea kupoteza maisha wakati bibi yake akiwa kwenye shughuli zake za kuuza chakula.

Wakati tukio hilo la kusikitisha linatokea bibi wa binti huyo alikuwa kwenye shughuli zake za kuuza chakula ambapo hurudi usiku wa saa saba ndipo akakuta mjukuu wake ameshafanyiwa tukio hilo la kusikitisha na kupoteza fahamu hadi alipompeleka hospitali na kuthibitika kupoteza maisha.

  • https://cast3.asurahosting.com/proxy/jambocom/stream

Verified by MonsterInsights