
Mlipuko kando na bomba la mafuta lililoharibiwa na wezi wa mafuta umeua watu wasiopungua kumi na mbili kusini mashariki mwa Nigeria.
Uharibifu wa bomba, kisha vitendo haramu vya usafishaji wa mafuta kuyauza kinyume cha sheria, sababu za majanga ya ikolojia na ajali mbaya, zimeenea katika eneo la kusini la mafuta nchini Nigeria, mzalishaji mkubwa wa mafuta barani Afrika.
Mlipuko huo ulitokea usiku wa alhamisi kuamkia ijumaa katika jamii ya Rumuekpe, katika jimbo la Rivers, ambapo kunapita bomba la mafuta la Trans-Niger delta (TNP), hiyo kulingana na taarifa ya shirika lisilo la kiserikali la Youths and Environmental Advocacy Centre (TEAC).
Habari hii imethibitishwa na polisi wa eneo hilo kwenye taarifa yake.