
Mlinzi wa Paris Saint-Germain, Achraf Hakimi ameshtakiwa kwa ubakaji na waendesha mashtaka wa Ufaransa, polisi nchini Ufaransa imeeleza leo ijumaa.
Mchezaji huyo wa kimataifa wa Morocco alishtakiwa na mwanamke mwenye umri wa miaka 24 ambaye alitoa malalamiko kwa polisi jumapili, februari 26.
Baada ya malalamiko ya awali, PSG ilitoa taarifa kwa vyombo vya habari vya Ufaransa ikimuunga mkono Hakimi, ikisema imekanusha vikali shutuma hizo na inaamini haki ni ya Hakimi na kuongeza kuwa PSG ni taasisi inayokuza heshima na imestaarabika ndani na nje ya uwanja.
Hakimi alikuwa mchezaji muhimu wa Morocco ilipofika nusu fainali ya kombe la dunia mwishoni mwa mwaka jana, na pia ni mchezaji muhimu wa mabingwa wa Ufaransa PSG.