fbpx

Miili kutoka makaburini yasombwa mafuriko Msumbiji

Miili kutoka kwenye makaburi kwenye kingo za mto Umbeluze karibu na mji mkuu wa Msumbiji, Maputo, imesombwa na mafuriko na kuenea katika mashamba ya watu.

Picha za Televisheni zilionesha madhara ya maji yanayochafuka ambayo yalifurika vitongoji vingi katika wilaya ya Boane, takribani kilomita 25 kusini-magharibi mwa mji mkuu, na kwingineko. Miili iliyotawanyika inaripotiwa kuhatarisha afya ya umma.

Wanajamii walitumia siku ya jumamosi na jumapili kukusanya maiti. Makaburi yaliyoathiriwa zaidi ni ya miongo mitatu na yana makaburi mengi ambayo hayajatambuliwa.

Kimbunga cha kitropiki freddy kilipiga nchini humo siku ya ijumaa na kusababisha mafuriko makubwa Katika eneo lote

  • https://cast3.asurahosting.com/proxy/jambocom/stream

Verified by MonsterInsights