fbpx

Messi atishiwa kifo kwa bunduki dukani kwa wakwe zake

Watu wawili wenye silaha wamefyatua risasi zaidi ya kumi na kuacha ujumbe wa vitisho kwa nyota wa soka wa Argentina, Lionel Messi katika uvamizi wa duka kubwa la wakwe zake mjini Rosario, Argentina. 

Maafisa wa vyombo vya mahakama wa mji wamelielezea tukio hilo limelotokea asubuhi ya jana alhamisi na kulitaja kuwa ni shambulizi la kigaidi.

Sambamba na shambulio hilo, watu hao waliacha pia ujumbe wa maandishi kwa mwanasoka huyo wa kulipwa  kwenye duka hilo, unaosomeka “Messi, tunakusubiri.” ujumbe huo umemlenga pia mwanasiasa wa eneo hilo, meya wa Rosario Pablo Javkin, ukidai kuwa yeye ni mfanya magendo wa dawa za kulevya na angemtunza Messi. Hakuna aliedhurika na shambulizi hilo hadi sasa.

Messi, ambaye ana nyumba huko Rosario na hutembelea familia mara kwa mara, hadi sasa hajatoa kauli yoyote juu ya tukio hilo.

Akiwa anatambuliwa kama mwanasoka bora zaidi wa wakati wote ,akiwa na miaka 35 sasa alishinda tuzo ya mchezaji bora wa kiume wa Fifa mapema wiki hii mbali na kuiongoza timu ya taifa ya Argentina na kutwaa kombe la dunia mwaka jana nchini Qatar baada ya kushindwa kulinyakua kwa miongo kadhaa.

  • https://cast3.asurahosting.com/proxy/jambocom/stream

Verified by MonsterInsights