
Mchimbaji mdogo aliyeifahamika kwa jina moja la Elias anaekadiriwa kuwa na umri wa miaka 29 hadi 30 aliekuwa nafanya kazi kwenye machimbo ya Magema yaliyopo kata ya Mtakuja halmashauri yam ji Geita amefariki dunia baada ya kuangukiwa na tufe la jiwe ambalo wenzie walikuwa wakiliponda wakiwa juu ya shimo alilokuwepo.
Wakiongelea gukio hilo baadhi ya wachimbaji wa maeneo hayo wanasema mchimbaji huyo alikuwa ndani ya duara akitoa mawe yanayosadikika kuwa na Dhahabu nje ya shimo, huku kifo chake kimetokana na walio nje ya shimo kuponyokwa na Jiwe walilokuwa wakilivunja.