fbpx

Mcheza Tennis, Andy Murray atinga robo fainali Qatar

Mchezaji wa Tennis kutokea Uingereza, Andy Murray ameendeleza ubabe wake kwa ushindi mkubwa dhidi ya mjerumani, Alexander Zverev na kutinga robo fainali ya michuano ya Tennis ya wazi ya Qatar.

Murray amemshinda Alexander jumla ya seti 7-6 za 7-5, 2-6, na 7-5 baada ya mechi kali kwa saa tatu mjini Doha nchini qatar. Ulikuwa ushindi mwingine wa kishindo kutoka kwa Murray katika mwaka mmoja ambapo ushindi wake wote umekuja katika hali ya kushangaza.

Kwingineko, kwenye michuano ya Rio Open nchini Brazil, mchezaji namba moja na kipenzi cha Uingereza, Cameroon Norrie ametinga robo fainali kwa ushindi wa seti 7-5 na 7-5 dhidi ya Thiago Monteiro wa Brazil.

  • https://cast3.asurahosting.com/proxy/jambocom/stream

Verified by MonsterInsights