
Katika ngumi Ratiba ya mashindano ya 13 ya IBA ya ubingwa wa dunia yatafunguliwa leo Alhamisi mjini New Delhi, Tanzania ikiwakilishwa na mabondia wawili.
Beatrice Nyambega atafungua dimba kwa mabondia wa Tanzania kesho Ijumaa kwenye mashindano ya ngumi ya dunia kwa wanawake yatakayofunguliwa kesho nchini India.
Beatrice atacheza na mwenyeji, Jasmine Jaismine kwenye uzani wa light kilogramu 60 kuanzia saa 9.30 alasiri ya Tanzania.
Mtanzania mwingine, Rahma Maganga atapanda ulingoni Jumamosi dhidi ya Mkenya,Kwenye uzani wa Minimum kilogramu 48.