fbpx

Marekani yaongeza msaada wa kijeshi nchini Somalia

Marekani imeongeza msaada wake wa kijeshi kwa nchi ya Somalia wakati taifa hilo likipiga hatua katika kukabiliana na mtandao wa kigaidi wa Al Gaida ilioutaja kuwa mbaya zaidi ulimwenguni.

Kwa mujibu wa shirika la habari la ap, tani 61 za silaha zimewasili kwenye mji mkuu wa Mogadishu  ambazo Marekani kupitia taarifa yake imesema kwamba ni za kusaidia kwenye vita vya kihistoria vinavyoongozwa na jeshi la Somalia, dhidi ya wanamgambo wa Al Shabab, likiwa limekomboa vijiji kutoka mikononi mwao tangu Agosti mwaka jana.

Kwenye taarifa tofauti ya pamoja, washirika wengine wakuu wa usalama,Qatar, Uturuki, UAE na Uingereza, pia wamesema kwamba watasaidia kwenye juhudi za Somalia za kudhibiti silaha, hatua itakayopelekea baraza la usalama la umoja wa mataifa kuondoa vikwazo vya kutouziwa silaha kwa taifa hilo.

Mwaka uliopita, serikali ya Somalia chini ya Rais Hassan Sheikh Mohamud ilitangaza vita dhidi ya maelfu ya wanamgambo wa Al Shabab ambao kwa miongo kadhaa wamedhibiti maeneo kadhaa na kufanya mashambulizi mabaya, wakati wakitumia migawanyiko iliyopo baina ya koo na kujipatia mamilioni ya dola kila mwaka wakijitahidi kubuni taifa la kiislamu.

  • https://cast3.asurahosting.com/proxy/jambocom/stream

Verified by MonsterInsights