fbpx

Marekani: Albamu mpya ya rapa Coolio imetoka baada ya kifo chake

Rapa Coolio

Albamu mpya ya muziki wa rapa Coolio imeachiwa mwaka huu ikiwa na nyimbo mpya alizokuwa akifanyia kazi siku chache kabla ya kifo chake.

“Long Live Coolio” ni albamu ya kwanza kutolewa baada ya kifo chake na singo ya kwanza “TAG ‘You It,’” imetoka jana Ijumaa ikiwa imemshirikisha Too $hort na DJ Wino.

Rapa huyo aliyepata umaarufu kutokana na ngoma zake za “Gangsta’s Paradise” alikufa kutokana na mshtuko wa moyo mnamo Septemba 28, 2022, akiwa na umri wa miaka 59.

Coolio alishinda Grammy ya onyesho bora zaidi la rap la solo la “Gangsta’s Paradise,” ya 1995.

  • https://cast3.asurahosting.com/proxy/jambocom/stream

Verified by MonsterInsights