
Mamba wawili waosadikiwa kushambulia watu Ziwa Victoria wameuawa katika Kata ya Nyakasasa Halmashauri ya Buchosa wilayani Sengerema, Mkoa wa Mwanza.
Zoezi la kuwanasa mamba hao limeendeshwa na maofisa Taasisi ya Utafiti wa Wanyamapori Tanzania iliyoko chini ya Wizara ya Maliasili na Utalii na hivi karibuni walimshambulia mtu mmoja kisha kupoteza maisha kwenye Kijiji cha lugata kisiwani Kome.