
Naibu Waziri wa Utamaduni, Sanaa na Michezo, Hamis Mwinjuma ameagiza makampuni na maeneo yanayotumia kazi za Sanaa na ubunifu kujinufaisha kibiashara kuhakikisha kuwa yanalipa mirabaha na madeni ya nyuma yanayodaiwa huku akiiagiza Ofisi ya Hakimiliki Tanzania (COSOTA) iwachukulie hatua za kisheria ikiwemo kuwafikisha Mahakamani wote waliokaidi kulipa.
Naibu Waziri Mwinjuma ametoa maagizo hayo alipofanya ziara ya kikazi katika ofisi za COSOTA kwa ajili ya kujionea shughuli zinazofanywa na ofisi hiyo.