fbpx

Majimbo sita yapinga matokeo ya uchaguzi Nigeria

Majimbo sita nchini Nigeria siku ya ijumaa yaliiomba mahakama ya juuu kufutilia mbali matokeo ya uchaguzi wa rais uliomalizika hivi punde, mgeuko wa hivi punde Katika changamoto kadhaa zinazokabili ushindi wa chama tawala Katika kura hizo.

Majimbo hayo yakiongozwa na magavana katika chama kikuu cha upinzani kilichoshika nafasi ya pili Katika uchaguzi wa mwishoni mwa juma lililopita yanaishutumu tume ya uchaguzi ya Nigeria kwa kushindwa kufuata kanuni ya sheria zake za uchaguzi Katika kuendesha kura na kutangaza mshindi, kulingana na nyaraka za mahakama.

Matokeo ya uchaguzi kutoka kwa vitengo 176,000 vya kupigia kura yanahitajika kutumwa kwenye tovuti ya tume, jambo ambalo upinzani unasema halikufanyika.

Bola Tinubu wa chama tawala alipata 37% ya kura ya kushinda uchaguzi huo, ambapo wagombea wengine akiwemo mgombea wa pili Atiku Abubakar na mshindi wa tatu Peter Obi wanasema watalipinga mahakamani.

  • https://cast3.asurahosting.com/proxy/jambocom/stream

Verified by MonsterInsights