
Mahakama ya kimataifa ya uhalifu wa kivita (ICC) imetoa hati ya kukamatwa kwa rais wa Urusi Vladimir Putin.
Mahakama ya ICC inadai kuwa anahusika na uhalifu wa kivita, ikiwa ni pamoja na kuwahamisha watoto kutoka Ukraine kwenda Urusi kinyume cha sheria.
Imesema uhalifu huo ulifanyika nchini Ukraine kuanzia tarehe 24 Februari 2022 – wakati Urusi ilipoanzisha uvamizi wake kamili.
Moscow imekanusha madai ya uhalifu wa kivita wakati wa uvamizi huo.
Mahakama ya ICC imemshtaki Bw. Putin kwa kuhusika katika kuwafukuza watoto, na imesema ina sababu za kuridhisha kuamini kuwa alifanya vitendo hivyo moja kwa moja, pamoja na kufanya kazi na wengine.