fbpx

Mafunzo ya ujasiriamali kwa wanawake yaanza Bariadi

Mkuu wa wilaya ya Bariadi, Simon Simalenga amefungua mafunzo ya ujasiriamali kwa vikundi 56 vya wanawake, vijana na watu wenye ulemavu ikiwa ni maandalizi ya kutoa mikopo ya asilimia 10 ya mapato ya ndani ya halmashauri ya mji wa Bariadi.

Amewahakikishia washiriki wa mafunzo hayo kuwa serikali wilayani humo kupitia halmashauri zake za Bariadi mji na halmashauri ya wilaya ya Bariadi imejipanga kutoa mikopo Zaidi kwa makundi hayo ikiwa ni utelekezaji maagizo ya serikali ya awamu ya sita chini ya Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan.

Kwa mujibu wa Simalenga mpaka sasa halmashauri ya mji wa Bariadi pekee imeshatoa mikopo kwa wanufaika 2,655 ambao wamepokea mikopo ya jumla ya shilingi 1, 054,284,000 ambapo katika makusanyo ya julai mpaka disemba 2022 serikali halmashauri itatoa mikopo ya shilingi 244,170,000 ikiwa ni asilimia 10 ya makusanyo kwa kipindi hicho katika ufunguzi wa mafunzo hayo mkuu huyo wa wilaya amewataka washiriki wa mafunzo kuzingatia sheria, kanuni na taratibu katika urejeshaji wa mikopo hiyo na kuondokana na dhana kwamba fedha hizo ni za bure kwasababu kwa kutokuzirejesha kunawanyima fursa ya mikopo watu wengi zaidi.

Ibara ya 24(b) Katika ukusara wa 20 wa ilani ya uchaguzi ya chama cha mapinduzi ya mwaka 2020/2025 chama hicho kimeielekeza serikali kutoa asilimia 10 ya makusanyo kwa kila halmashauri hapa nchini na kutoa mikopo kwa makundi ya wanawake, vijana na watu wenye ulemavu ili kujikwamua kiuchumi.

  • https://cast3.asurahosting.com/proxy/jambocom/stream

Verified by MonsterInsights