fbpx

Maelfu ya wafuasi wa upinzani waandamana Senegal

maandamano

Maelfu ya wafuasi wa kiongozi wa upinzani wa Senegal, Ousmane Sonko wameaandamana mjini Dakar ikiwa ni siku ya kwanza kati ya maandamano ya siku kadhaa huku nchi hiyo ikijiandaa kwa uchaguzi chini ya mwaka mmoja.

Mvutano unaongezeka kabla ya upigaji kura katika nchi inayoonekana kuwa mhimili mkuu wa kidemokrasia katika eneo hilo, huku kukiwa na uvumi kuwa Rais Macky Sall anaweza kukwepa katiba na kutafuta muhula wa tatu wa urais.

  • https://cast3.asurahosting.com/proxy/jambocom/stream

Verified by MonsterInsights