
Maandamano ya kupinga uamuzi wa Rais wa Ufaransa Emmanuel Macron kulazimisha mswada wa kuongeza umri wa kustaafu kutoka miaka 62 hadi 64 kupitia bunge bila kura yalitatiza shughuli za usafiri, ukusanyaji wa taka na vyuo vikuu mjini Paris huku wapinzani wa mabadiliko hayo wakidumisha azimio lao la kutaka serikali ibadilishe uamuzi huo.
Wafanyakazi wa usafi wa mazingira walizuia kiwanda cha kukusanya taka ambacho ni nyumbani kwa kichomaji taka kikubwa zaidi barani Ulaya ili kusisitiza azimio lao, na wanafunzi wa vyuo vikuu walitoka nje ya kumbi za mihadhara ili kujiunga na migomo. Viongozi wa chama chenye ushawishi mkubwa cha CGT walitoa wito kwa watu kuacha shule, viwanda, viwanda vya kusafisha na maeneo mengine ya kazi.
Viongozi wa Leba nchini Ufaransa waliitisha maandamano mapya kufuatia tangazo hilo, huku maelfu ya watu wakikusanyika Paris na miji mingine kadhaa nchini Ufaransa alhamisi jioni. Pia, Philippe Martinez, mkuu wa chama cha wafanyakazi cha CGT aliitisha migomo na maandamano zaidi.