fbpx

Kujengwa kwa kituo cha afya kuokoa wakazi 4000 Shinyanga

Zaidi ya wakazi 4000 wa kata ya Igwamanoni katika halmashauri ya Ushetu wilayani Kahama mkoani Shinyanga wanatarajia kuondokana na tatizo la kutembea umbali wa kilomita 30 kutafuta huduma za matibabu baada ya serikali kujenga kituo cha afya kipya kwa gharama ya shilingi milioni 500 ambacho ujenzi wake umefikia asilimia 95.

Kukamilika kwa kituo cha afya Igwamanoni kitawanufaisha wakazi zaidi ya 4000 huku akinamama wajawazito na watoto wakiwa ni wanufaika wa huduma hizo. Esta Mabere na Magreth Mashauri ni baadhi ya wakazi wa kata hiyo wamepaza sauti kwenye mkutano wa hadhara Mbunge wa jimbo la Ushetu Emmanuel Cherehani wakati akiwasilisha taarifa ya utendaji kwa kipindi cha mwaka mmoja wa uongozi wake.

Gagi Lala ni mwenyekiti wa halmashauri ya Ushetu amesema kwa sasa kituo hicho kinahitaji miundombinu ya umeme na maji huku Mbunge wa jimbo la Ushetu Emmanuel Cherehani akikemea tabia ya baadhi ya watumishi wa afya kuwatoza faini wajawazito wanaojifungulia nyumbani.

Kwa upande wake Thomas Muyonga mwenyekiti wa CCM wilaya ya Kahama ameawataka viongozi wa serikali kusimamia kikamilifu sekta ya afya hususani upande wa bima ya CHF ambayo inaongoza kwa malalamiko vijijini.

  • https://cast3.asurahosting.com/proxy/jambocom/stream

Verified by MonsterInsights