fbpx

Kongo yapewa msaada wa kibinadamu

Tani 35 ya msaada wa kibinadamu umewasili leo asubuhi mjini Goma, mashariki mwa DRC kuwasaidia maelfu ya wakimbizi waliokimbia makaazi yao kutokana na vita kati ya waasi wa M 23 na wanajeshi wa serikali. 

Msaada huo  kutoka umoja wa Ulaya, unatarajiwa kuwafikia watu 800,000 ambao wanakabiliwa na hali mbaya ya kibinadamu tangu kuanza kwa vita hivyo, kwa mujibu wa umoja wa mataifa. 

Huu utakuwa ni msaada wa pili, baada ya EU kutuma msaada wa kwanza machi 10, siku chache baada ya rais wa Ufaransa kutembelea nchi hiyo na kuahidi kuwa mataifa ya Ulaya yangetuma msaada huo. 

  • https://cast3.asurahosting.com/proxy/jambocom/stream

Verified by MonsterInsights