
Wizara ya uwekezaji, viwanda na biashara kwa kushirikiana na umoja wa Ulaya pamoja na sekta binafsi ya Tanzania imeandaa kongamano la biashara kati ya Tanzania na nchi za umoja wa Ulaya linalotarajiwa kufanyika kuanzia tarehe 23 hadi 24 Februari mwaka huu.
Kongamano hilo linatarajiwa kujumuisha zaidi ya washiriki 600 kutoka nchi za umoja wa Ulaya na Tanzania linalenga kuwaunganisha washiriki hao ili kuwawezesha kubadilishana uzoefu, kushirikiana na watoa maamuzi na kukutana na wawekezaji wanaofaa pamoja na kujenga uelewa kuhusu fursa za uwekezaji zilizopo kwa sekta ya umma na binafsi ambapo, hati za makubaliano mbalimbali ya uwekezaji baina ya Tanzania na nchi za umoja wa Ulaya zitatiwa saini.
Kongamano hilo linatarajiwa kuzinduliwa rasmi na makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania mheshimiwa Dkt. Philip Mpango, akimwakilisha mheshimiwa Dkt. Samia Suluhu Hassan, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na litafungwa rasmi na Rais wa serikali ya Mapinduzi Zanzibar, mheshimiwa Dkt. Hussein Mwinyi ambaye atashuhudia utiaji saini wa mikataba ya fedha na hati za makubaliano.
Aidha, wafanyabiashara na wawekezaji kutoka Tanzania mtumie fursa hii vizuri kuendeleza na kukuza biashara yenu kwa kujifunza mbinu mpya za kibiashara, kupata wabia na masoko ya bidhaa zetu nje ya nchi