fbpx

Kombe la FA kukamilisha hatua ya 16 bora kwa michezo minne

Michuano ya kombe la FA nchini Uingereza iliendelea hapo jana kwa michezo minne ya kukamilisha hatua ta 16 bora ambapo

Southampton wakiwa nyumban St Marys wamekubali kipigo cha mabao 2-1 mbele ya Grimsby, Burnley wakiwa nyumbani wametakata kwa ushindi wa bao 1-0 mbele ya Fleetwood, mashetani wekundu Manchester United wametakata pia nyumban kwa ushindi wa magoli 3-1 mbele ya West Ham united kutoka london, mchezo wa mwisho Sheffield United wameiondosha Tottenham baada ya ushindi wa bao 1-0

Baada ya michezo ya jana droo ya robo fainali imefanyika na michezo robo fainali itapigwa march 18 ambapo

Robo fainali ya kwanza Brighton watawaalika Grimsby Town , robo fainali ya pili Sheffield United watawaalika Blackburn Rovers, mchezo wa tatu Manchester City watakuwa nyumban kuwakaribisha Burnley na mchezo wa mwisho katika hatua ya robo fainali Manchester United watakuwa nyumban kuwakabili Fulham michezo yote itapigwa saa 4:45 usiku

Ligi kuu EPL iliendelea pia kwa michezo miwili hapo jana vinara arsenali wameendelea kujiimarisha kileleni mwa EPL baada ya ushindi mnono wa magoli 4-0 mbele ya everton, mchezo wa pili liverpool wakiwa nyumban anfield wakawalaza 2-0 wolvehampton na kupanda hadi nafasi ya 6.

  • https://cast3.asurahosting.com/proxy/jambocom/stream

Verified by MonsterInsights