
Rais wa Malawi, Lazarus Chakwera ametangaza wiki mbili za maombolezo ya kitaifa kwa zaidi ya watu 200 waliofariki kutokana na Kimbunga Freddy, kilichoikumba nchi hiyo wiki hii.
Hatimaye kimbunga hicho kimefifia baada ya kusafiri kilomita 8,000 kuvuka bahari ya Hindi, na kubadili mkondo wake na kupiga Afrika kwa mara ya pili na kuweka rekodi isiyo rasmi ndefu zaidi ya kitropiki duniani.