fbpx

Kilimo cha Kahawa kukumbwa na mnyauko wilayani Ngara

Baadhi ya wakulima wa Kahawa wilayani Ngara wamesema kuwa kilimo cha Kahawa kimeanza kukumbwa na changamoto ya  ugonjwa wa munyauko hali ambayo  itasababisha mavuno katika msimu ujao kutokuwa makubwa.

Wakizungumza na Jambo FM wamesema kuwa ikiwa chama cha Ngara Farmers hakitachukua hatua za makusudi uwezekano wa  wakulima kuuza kahawa ya kutosha kwenye chama hicho utakuwa mdogo.

Wamesema kuwa matarajio yaliyowekwa ya kununua kilo milioni mbili utakuwa mdogo kutokana na magonjwa ambayo yameanza kujitokeza kwa  wakulima  na kuomba maafisa ugani waanze kufika kwa wakulima  ili kutafuta ufumbuzi wa changmoto ya magonjwa hayo.

Awali meneja wa chama hicho wilayani Ngara, Zefania Munyonyera amesema kuwa msimu ujao mavuno ya kahawa yatakuwa makubwa  ambayo yatawezesha wakulima kupata fedha ya kutosha lakini pia bei ya kahawa itakuwa bora kuliko msimu uliopita ikiwa ni pamoja na kununua kahawa nje ya wilaya hiyo

  • https://cast3.asurahosting.com/proxy/jambocom/stream

Verified by MonsterInsights