
Wizara ya elimu nchini Kenya imeanzisha msako mkali dhidi ya kile ilichotaja kuwa kupenya kwa ajenda ya mahusiano ya jinsia moja ( LGBTQ) shuleni.
Kamati tayari imeundwa kushughulikia masuala ya LGBTQ shuleni, waziri alisema, na kupendekeza jukumu lake linaweza kujumuisha kupitia upya fasihi ya shule ikiongozwa na askofu mkuu kutoka kanisa la kianglikana nchini Kenya.
Mapenzi ya jinsia moja bado ni haramu lakini mitazamo dhidi ya mashoga imekuwa migumu baada ya uamuzi wa mwezi uliopita wa mahakama ya juu kushikilia haki ya jumuiya ya mashoga kusajili chama.