
Baada ya pambano lake la mwisho kule nchini Kenya dhidi ya bondia wa Kenya, Daniel Wanyonyi bondia machachari Karim Khalid Saidi “Karim Mandonga” tarehe 25/03/2023 atakuwepo tena nchini Kenya kwenye pambano dhidi ya bondia kutoka Uganda.
Mandonga ameeleza kwamba tayari ameanza maandalizi mapema na kutambulisha mapigo mapya atakayokwenda kutumia dhidi ya bondia raia wa Uganda.