
Real Madrid wanatajwa kufikia makubaliano ya kuongeza mkataba mpya na mshambuliaji na Karim Benzema ambae kandarasi yake huko Santiago Bernabeu inafikia ukomo msimu huu wa joto.
Karim, mshindi wa tuzo ya Ballon d’Or kwa sasa, aliifungia Madrid bao la ushindi katika ushindi wa 1-0 dhidi ya Liverpool Jumatano usiku wa kuamkia leo na kufanikiwa kutinga hatua ya robo fainali Ligi ya Mabingwa barani ulaya inaelezwa kuwa amekubali kusaini kandarasi mpya ya mwaka 1.