
Kamati ya kudumu ya bunge ya Nishati na Madini imeridhishwa na maendeleo ya ujenzi wa mradi wa Bomba la Mafuta ghafi la Afrika Mashariki linalojengwa kutoka nchini Uganda hadi Tanga, Tanzania lenye urefu wa kilomita 1,443.
Mwenyekiti wa kamati hiyo ya Bunge, Dunstan Kitandula amekiri kuridhishwa na kasi ya ujenzi wa mradi huo, wakati wa ziara ya kukagua utekelezaji wa mradi huo wa bomba la Mafuta ghafi la Afrika Mashariki kwa upande wa Tanzania.