
Kamati ya kudumu ya Bunge ya Maji na Mazingira imeanza ziara yake leo tarehe 15 Machi, 2023 katika Wilaya ya Kahama, Mkoani Shinyanga na kukagua Miradi miwili ya Kagongwa, Isaka kwenda vijiji vya Kilimbu, Jana, Butondolo na Itogwanholo na mradi wa maji wa Tinde hadi Shelui ambayo inasimamiwa na Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Shinyanga (SHUWASA) pamoja na Wakala wa Maji na Usafi wa Mazingira Shinyanga (RUWASA).
Miradi hiyo miwili inapokea maji kutoka mradi mkubwa unaotoka ziwa Victoria unaosimamiwa na Mamlaka ya Majisafi Kahama Shinyanga (KASHWASA).