
Taharuki imezuka kwa wakazi wa kitongoji cha CCM-Senta kijiji cha Lwamgasa, kata ya Lwamgasa wilayani Geita baada ya kaburi alipozikwa mtoto wa miaka miwili kutoka familia ya Dismass John kufukuliwa na watu wasiojulikana na kuacha taharuki kwa majirani.
Shuhuda wa mazishi ya mtoto huyo ambaye ni mkazi wa kitongoji hicho, Isack William amesema wanashangazwa na tukio hilo kwani halijawahi kutokea kijijini hapo.