
Meneja wa As Roma, Jose Mourinho ametishia kuchukua hatua za kisheria dhidi ya afisa namba nne “fourth official” wa mchezo wa jana kati ya As Roma na Cremonese Marco Serra baada ya mreno huyo kutolewa nje kwa kadi nyekundu katika mchezo wa serie A ambao Roma walichapwa 2-1 na Cremonese jana jumanne.
Sio kwa mara ya kwanza msimu huu, bosi huyo wa Roma kupewa onyo na mwamuzi Marco muda mfupi baada ya mapumziko na timu yake ikiwa nyuma kwa bao 1-0. “nina hisia, lakini sio wazimu,” mourinho aliiambia chombo cha habari cha dazn. Na kuongeza kuwa “ili kuguswa jinsi alivyofanya, lazima kitu kitokee kwanza.
Na kuongeza kuwa anahitaji kuelewa ikiwa anaweza kuchukua hatua zozote za kisheria dhidi ya mwamuzi huyo.