
Meneja wa Ligi kuu soka Tanzania TPLB, Jonathan Kassano ameteuliwa na shirikisho la soka barani Afrika CAF kuwa mratibu yaani General Coordinator wa mchezo wa hatua ya makundi ligi ya mabingwa Afrika kati ya Al Hilal Omdurman ya Sudan dhidi ya Mamelodi Sundowns ya Afrika Kusini utakaochezwa machi 18, 2023 nchini Sudan.
Mjumbe wa kamati ya utendaji ya shirikisho la soka nchini Tanzania TFF, Khalid Abdallah ameteuliwa na shirikisho la soka barani Afrika CAF kuwa kamishna wa mchezo wa hatua ya makundi ligi ya mabingwa Afrika kati ya Zamalek SC ya Misri watakapowavaa Esperance .Sportive de Tunnis ya Tunisia utakaochezwa machi 7, 2023 pia meneja mashindano wa shirikisho la soka nchini Tanzania TFF.
Baraka Kizuguto ameteuliwa na CAF kuwa mratibu yaani General Coordinator wa mchezo wa hatua ya makundi ligi ya mabingwa afrika kati ya Mamelodi Sundowns (Afrika Kusini watakapo wavaa Al Ahly SC Misri machi 11, 2023.