
Rais wa Marekani, Joe Biden amepongeza uamuzi wa mahakama ya kimataifa ya uhalifu wa kivita, ICC uliotoa hati ya kukamatwa kwa Rais mwenzake wa Urusi, Vladimir Putin.
Mahakama ya ICC ilimshutumu Rais Putin kwa kufanya uhalifu wa kivita nchini Ukraine jambo ambalo Rais Biden alisema kiongozi huyo wa Urusi “alifanya kwa uwazi, Madai hayo yanaangazia uhamishaji haramu wa watoto kutoka Ukraine hadi Urusi tangu uvamizi wa Moscow mwaka 2022.