
Rais wa FIFA, Gianni Infantino amechaguliwa tena kuendelea kuongoza shirikisho hilo hadi mwaka 2027 baada ya kusimama kama mgombea pekee kwenye uchaguzi uliofanyika leo Machi 16 nchini Rwanda.
Akizungumza baada ya uchaguzi huo amesema nikimnukuu “Kuwa Rais wa FIFA ni heshima kubwa, ninashukuru na kuguswa na sapoti yenu. Nitaendelea kuhudumu FIFA, nitautumikia mpira dunia nzima, nitahudumia mashirikisho yote 211 ya FIFA”