fbpx

Gavana abomoa barabara kuzuia tume ya uchaguzi Nigeria

Yahaya Bello ambaye ni Gavana wa Jimbo la Kogi nchini Nigeria, anadaiwa kuharibu barabara tano zinazoelekea mji wa nyumbani kwa Natasha Akpoti (mgombea wa useneta katika chama cha upinzani) ili kuzuia maafisa wa Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi Nigeria (INEC) kufika huko.

Gavana huyo alidai kuwa sababu ya uchimbaji wa baadhi ya barabara ni hatua ya awali ili kuwazuia magaidi kufikia lengo lao la kufanya ugaidi katika Jimbo la Kogi.

Wananchi wa jimbo la Kogi walifanya uamuzi wa kutengenezo barabara hizo wenyewe ili tume ya uchaguzi iweze kufika katika jimbo hilo.

  • https://cast3.asurahosting.com/proxy/jambocom/stream

Verified by MonsterInsights