fbpx

Ewura yatangaza bei mpya ya mafuta

Mamlaka ya udhibiti wa huduma za nishati na maji (Ewura) imetangaza bei mpya za mafuta zitakazotumika kuanzia leo jumatano, Machi 1, 2023 huku bei ya petrol na dizeli zikipaa ikilinganishwa na Februari.

Katika taarifa hiyo iliyotolewa na Mkurugenzi mkuu wa Ewura, Dkt James Mwainyekule imeonyesha kuwa katika jiji la Dar es Salaam bei ya mafuta ya petroli itauzwa sh2,960 mwezi huu ikilinganishwa na sh2,819 ya Februari.

Hali kadhalika, bei ya dizeli imeongezeka kidogo kutoka sh3,105 Februari hadi sh3,130 mwezi huu sawa na ongezeko la sh25.

Wakati bei hizo zikipaa katika jiji la Dar es Salaam, hali ni tofauti kwa mikoa ya kaskazini ikijumuisha Tanga, Kilimanjaro, Arusha na Manyara ambao mafuta ya dizeli yamepungua kwa sh64 kwa lita kutoka sh2,967 Februari hadi sh2,903 mwezi huu.

Huku kwa upande wa dizeli kwenye mikoa hiyo imeshuka kwa sh209 kutoka sh3,340 Februari hadi sh3,131 mwezi huu.

  • https://cast3.asurahosting.com/proxy/jambocom/stream

Verified by MonsterInsights