fbpx

EWURA yahamasisha uwekezaji gesi ya LPG nchini

Mamlaka ya Udhibiti wa Huduma za Nishati na Maji ( EWURA), imeendelea kuwahamasisha Watanzania na wawekezaji wa ukanda wa Afrika Mashariki kuwekeza katika uhifadhi wa gesi ya kupikia (LPG) ili kukuza zaidi matumizi ya nishati hiyo nchini.

Meneja Biashara ya Petroli wa EWURA, Kemilembe Kafanabo, ametoa hamasa hiyo wakati akiwasilisha mada kuhusu usalama, ubora,na uhimili wa gesi ya kupikia kwenye kongamano la wadau wa gesi ya kupikia ( LPG) linalofanyika katika hoteli ya Johari Rotana, jijini Dar es Salaam kuanzia tarehe 15-16 Machi 2023.

  • https://cast3.asurahosting.com/proxy/jambocom/stream

Verified by MonsterInsights