fbpx

Erling Haaland avunja rekodi ya ufungaji bora

Erling Haaland

Baada ya mshambuliaji wa Manchester City, Erling Haaland hapo jana kufunga mabao 5 kwenye ushindi wa mabao 7-0 walioupata Man City dhidi ya RB Leipzing kwenye mchezo wa ligi ya mabingwa Ulaya, mshambuliaji huyo ameweka na kuvunja rekodi kadhaa.

Haaland amekuwa mchezaji wa tatu kufunga mabao 5, kwenye mchezo mmoja wa ligi ya mabingwa Ulaya anaungana na Lionel Messi aliyefanya hivyo mwaka 2012 na Luiz Adriano mwaka 2014.

Pia amefikisha idadi ya hat-tricks 5 msimu huu kwenye michuano yote, ikiwa ni hat-trick ya 3 zaidi ya mchezaji yoyote kwenye Ligi kubwa 5 barani Ulaya msimu huu 2022-23.

  • https://cast3.asurahosting.com/proxy/jambocom/stream

Verified by MonsterInsights