fbpx

EPRA imetangaza ongezeko la bei ya Petroli Kenya

Mkurugenzi mkuu EPRA, Daniel Kiptoo

Mamlaka ya Udhibiti wa Nishati na Petroli Kenya, EPRA imetangaza ongezeko la bei ya reja reja ya mafuta ya petroli kwa Ksh. 2 ya kenya.

Bei za mafuta iliyotolewa jana Jumanne, Machi 14, 2023, EPRA ilitangaza kuwa bei ya dizeli na mafuta taa kwa lita itasalia bila kubadilika kwa shilingi ya Kenya 162 na.145 Jijini Nairobi.

Kwa upande mwingine, gharama ya petroli itapanda hadi shilingi ya Kenya 179.20 kwa lita moja jijini Nairobi.na kuongeza kuwa serikali imetoa shilingi za Kenya 23.49 / kwenye kila moja lita ya Mafuta ya Taa ili kuwapa ahuaeni wananchi. Bei hizo mpya zitaanza kutumika kuanzia Machi 15, 2023 hadi Aprili 14, 2023

  • https://cast3.asurahosting.com/proxy/jambocom/stream

Verified by MonsterInsights