
Katika michezo mingine magoli matatu wa Engel Di Maria yameisaidia Juventus kutinga hatua ya 16 kwa ushindi Mujarrab wa magoli 3-0 mbele ya Nantes ugenini.
Bayer Levakusen walitakata ugenini kwa ushindi wa magoli 3-2 mbele ya Monaco wakisawazisha makosa ya kufungwa 3-2 nyumbani na kufanikiwa kushinda kwa penalty 10 – 8 Union Berlin wakaibuka ushindi wa magoli 3-1 mbele ya mabarobaro Ajax kutoka jiji la Amsterdam, nchini Uholanzi, As Roma ya Italia wakashinda 2-0 mbele ya Salzburg.
Licha ya ushindi wa magoli 2-0 lakini PSV Eindhoven walishindwa kupindua meza ya magoli 3-0 walipofungwa 3-0 mbele ya Sevilla wiki iliyopita nchini Hispania.
Mchezo mwingine Sporting CP waliwachapa bila huruma Mdtland magoli 4-0 na kusonga mbele kwa jumla ya magoli 5-1.