fbpx

‘Desturi zetu haziruhusu mapenzi ya jinsia moja’ – Museveni

Rais wa Uganda Yoweri Museveni amesema kuwa nchi za magharibi hazipaswi kulazimisha desturi zao kwa waafrika kwa kuhalalisha mapenzi ya jinsia moja.

Katika hotuba yake maalumu kwa bunge Rais ameongeza kuwa mapenzi ya jinsi moja ni kupotoka au kuondokana na kile kilicho cha kawaida.

Maoni yake yanakuja wakati ambapo kuna wimbi la chuki dhidi ya wapenzi wa jinsia moja linaloenea kote nchini humo na ukanda wa Afrika Mashariki.

Wanaharakati wa LGBTQ wanasema jumuiya yao imekabiliwa na unyanyasaji wa kimwili na mtandaoni katika wiki za hivi karibuni.

Mswada wa kupinga mapenzi ya jinsia moja uliwasilishwa katika bunge la Uganda mapema mwezi huu. Unatafuta kuifanya kuwa haramu kwa mtu yeyote kujitambulisha kama anayeshiriki mapenzi ya jinsia moja.

  • https://cast3.asurahosting.com/proxy/jambocom/stream

Verified by MonsterInsights